Vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimetangaza kuwa nchi hiyo inalenga kuimarisha uwezo wake wa nyuklia pamoja, kuimarisha idara yake ya ujasusi na jeshi la taifa hilo.
Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini, Korean Central News Agency (KCNA), liliripoti kuwa suala hilo lilijadiliwa katika mkutano wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya chama tawala uliofanyika hapo jana.
Korea Kaskazini iko chini ya vikwazo vikali vya kimataifa kutokana na mpango wake wa nyuklia.
0 Comments