Spika wa Bunge Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu amesema wageni zaidi ya 2226 wapo Arusha kwa ajili ya Mkutano wa 153 wa IPU ni 2226 ikiwemo Maspika 54, manaibu Spika takribani 38.

Amesema maandalizi yote ya Mkutano wa IPU yamefanywa na washirika wa ndani kwa kushirikiana na Bunge na baadhi ya sekta binfsi zilizopo Tanzania.

“Tunawakaribisha wageni wote, Dunia nzima ipo hapa Arusha kuja kuona watanzania tunaweza kufanya nini,” amesema.

Amesema Tanzania ipo tayari kwa ajili ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea jijini Arusha huku akisisitiza kwamba Tanzania imeendelea kuimarisha utawala bora.

Amesema Dira ya Taifa ya Mwaka 2050 imejumuisha program za kuimarisha Utawala Bora na kwamba Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza kwamba Dira ya Taifa itafanikiwa kwa kuendelea kuimarisha utawala, haki za kisiasa, haki za binadamu na demokrasia.

Mheshimiwa Spika alikuwa akingumza katika Mkutano Maalumu wa waandishi wa habari uliofanyika kabla ya ufunguzi rasmi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) jijini Arusha.