Wapiganaji tisa wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Libya wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa katika makabiliano ya kusambaratisha kundi la Islamic state kutoka kwa ngome yake ya Sirte, msemaji wa hospitali amesema, nashirika la habari la Associated Press kuripoti.
Wapinganaji hao walifariki kutokana na mashambulio ya bunduki zilizowalenga moja kwa moja, ama kwa mashambulio ya mabomu yaliyotegwa barabarani katika vita vya mapema wiki hii.
Sirte ni eneo ambalo aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alizaliwa kabla ya kuuawa na jeshi la muungano wa NATO mwaka 2011.
|
0 Comments