Mmeziona PETE?? bwana Habib na mkewe Monica wakiwaonyesha PETE wageni waalikwa na wote wanaowaangalia hivi sasa picha hizi,kwambaaaa Monica ni Mke halali wa bwana Habib,na Habib ni mume halali wa bi Monica.Ukitaka kwenda jela maisha ongea na mke au mume wa mtu uone cha moto.
Araamba Araaamba tenaa Haam Haaam Araaamba Araamba tena Haaaam haaaaamm..wacha weeee..
Flash time kwa maharusi wetu,kiukweli wali`shine ukumbini na kila mmoja aliwapongeza kwa kupendeza kwao.Hongereni sana maharusi .
Baada ya kulishana keki maharusi,waligawa keki kwa kila mtu aliyebahatika kufika ukumbina hapo.keki ilikuwa tanu kushinda maelezo.
Kuhusu msosi kwa kweli sina la kusema,maana ilikuwa ikitangazwa watu wakarudie chakula tena na tena kwa jinsi msosi ulivyokuwa mwingi sana.pichani bidada mwenye blue akiwasaidia maharusi wetu kwenyelmasuala mazima ya mambo ya MADIKODIKO.
Kila mmoja alikuwa kwa raha zake na kuongeza kwa raha zake moka kusema basiiii nimetosheka.
Mashostisho wakipiga menu yenye kila mchanganyiko wa mambo mazuri .
Wastaarabu wa Den Haag wakipata Flash time na huku brother Hasheem akishikilia vyema plate yake ya madikodiko.
Kuhusu Vinywaji kwa kweli kila mmoja aliondoka amefurahia huduma toka kwa vijana hawa.
Kaka wa bi Monica akipata Flash time na shemeji yake bwana Habib,pichani amewashikilia watoto wake na kulia kabisa ni dada wa bwana maarufu pale Almere ni bidada Fatma.
Kicheko cha ukweli toka kwenye Nafsi ambacho hakina unafiki toka kwa dada wa bwana harusi na kulia ni mmoja wa wageni waliotoka London kwa ajili ya shughulu hii,Mungu awazidishie kwa kila lililona heri kwao.
Flash time kwa kila aliyefika ukumbinipale.
Kabla ya kuwaaga maharusi wetu,madada toka nchini Uingereza walipata kumbukumbu nzurrii kwa maharusi wetu.
Raha ya harusi kama hii ukikutana na watu wazima kama hivi ujue hapatakuja kuharibika kitu.safi sana.
Mambo burrrdani mashostisho wakiendelea kumsikiliza Mc TONNY ``Sex Mama``hayupo pichani akiwajibika vilivyo kupanda show nzima ya harusi.
Celebrate toka Amsterdam Brother Chura kushoto akipata Flash time na bwana Habib
Mawifi waliotoka London na kuja Holland kushuhudia kaka yao anawaletea wifi nyumbani nao walipata Flash time na Maganga One.
Nasemaaa,mwenye wivu ajinyonge ila bi Monica alipendeza ..ebu mcheki kisha ubishe kama unapenda kubisha.
Kama kawa,ni urembo na warembo toka sehemu mbalimbali walikuwepo ukumbini hapo kushuhudia harusi ya bwana Habib na bi Monica
Shoto ni bidada wa dada Asha Baraka,kati ni Mya au mama Tareeq na aunt Jamillah,hii tunaita Flash time.
Kaka Tau kushoto,Mr n` Mrs Habib na bidada walipata picha ya pamoja kama kumbukumbu kwa siku ya leo
Mc Seki kushoto na brotherman ndani ya nyumba kushuhudia shughuli nzima ya harusi ya bwana Habib na bi Monica.
Ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa maharusi walipata picha za pamoja kama kumbukumbu za harusi hii
Kutoka kushoto ni Bachala,brother kaka,aunt Jamillah,brother kaka na HB wa Almere bwana Kabila.
Kapendeza hajapendezaaaa? Kapendezaaaaaaaaaa................................... Ahsanteni.
Kutoka kushoto mwenye shati jeusi ni Kamanda Kaseke,Brother James,Maganga One na Aliyekonga nyoyo za watu kwa burudani sawiaaa ukumbini hapo ni Dj Khatib toka Leiden Holland.
Eeehe wacha weee ni bidada Mariam na shost wake pembeni yani full kupendazaaa
Mke wa kaka Hasheem,toka Den Haag nchini Holland ni shemeji mama Tareeq au mama Warda,full kupendezaaa.
Maharuis wetu wakipata picha ya pamoja na ma MC wa Holland,kutoka kushoto ni Mc Seki ambaye kwa leo alikuwa off na kulia kabisa aliyeisherehesha harusi ya bwana Habib na kufana kiukweli mpaka mimi mwenyewe nimemkubali ni Mc SONNY ama almaarufu SEX MAMA...Siunamkcheki mwenyewee..
1 Comments
Jah Bless.
Tau