Rais Jakaya Mrisho Kikwete amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho kupisha uchaguzi kufanyika upya. Licha ya kujiuzulu lakini Rais Kikwete anataraji kuchaguliwa tena kwa kishindo kwani ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo ya Uenyekiti. Kufuatia kujiuzulu huko nafasi ya Uenyekiti imeshikiliwa kwa muda na Rais Mstaafu, Benjamini William Mkapa aliyeungwa mkono na wajumbe wote baada ya jina lake kupendekezwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake. Mbali na Mwenyekiti pia Sekretarieti yote ya chama hicho imejiuzulu na inasubiri kuchaguliwa tena baada ya uchaguzi kukamilika. Wadau, mnaonaje hili? Chanzo cha habari hizi ni HAPA |
1 Comments
RAIA WA MAREKANI NA UINGEREZA WASHIRIKI MKUTANO WA CCM DODOMA, WATUMIWA NAULI KUSHIRIKI MKUTANO NA KUPIGA KURA. ZILITUMWA TICKETS 40 KWA MKOA WA DIASPORA, UINGEREZA, CHINA, INDIA MAREKANI N.K DMV TICKETS 8.
CCM na JK wazivunja katiba za nchi na chama. Mwenyekiti wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete na wanachama wa CCM wamewaruhusu RAIA wa MAREKANI na Uingereza kupiga kura DODOMA. CCM na uongozi wake vimekuwa vikilifumbia macho swala la uraia pacha, hapo hapo inawatumia raia wa nchi nyingine pesa za walipa kodi kwa ajili ya nauli ili wapate political points.
Kanuni za katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na ya CCM haziruhusu mtu mwenye uraia ambao sio wa Tanzania kushiriki shughuri za kisiasa nchini (HATUNA DUAL CITIZENSHIP). Hawa ni raia wa Marekani ambao wameshiriki uchaguzi DODOMA
-Phanuel Peter Ligate (USA citizen)
-Faraja Isingo (Raia wa kuzaliwa Marekani, alizaliwa Oklahoma)
-Maftah ambaye ni mwenyekiti wa New york CCM (USA citizen)
-Bashiri (Huyu ni Raia wa Uingereza na Burundi)
Kama hawa watu wanakanusha hili. Waonyeshe HATI zao za kusafilia na ziwe na STAMP ya entry na exit…Marekani na Tanzania
Hawa ni Green card holders sheria haiwabani
-Benjamini Mwaipaja
-Elizabeth Luhanga
-Loveness Mamuya (Huyu mara ya mwisho alikua anafanya process za uraia wa Marekani hatuna uhakika kafikia wapi)
TUNAWASHANGAA CMM NA JK WANAVYO ENDESHA MAMBO YAO YA KISIASA KWA KUWA FUMBA MACHO WANACHMA WAO NA WANACHI NA KUTUMIA PESA ZA WALIPA KODI KUWALIPIA NAULI RAIA WA NCHI ZA WATU.