Tangazo hilo ilikuwa la John Okello, ambaye mpaka
mauti yanamfika haikufahamika kama alikuwa ni raia wa Kenya au Uganda.
Okello na msaidizi wake Engine walitoa amri ya kukamatwa kwa mawaziri wa
Serikali ya Sultan na kukataza watu kutembea.
Itakumbukwa kuwa usiku wa sherehe za Mapinduzi hayo Januari 11,
1964, Hayati Aman Karume alipelekwa mafichoni jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kumwepusha asikamatwe endapo mapinduzi hayo yasingefanikiwa.
Katika mwendelezo wa juhudi za kukikomboa kisiwa
hicho, mamia ya watu wenye asili ya Oman na Comoro walifukuzwa Zanzibar
ambapo watoto wadogo walipelekwa maeneo ya bandarini kuonana na baba zao
kwa ajili ya safari ya Oman.
Kazi iliyofuata ilikuwa ni kulinda mapinduzi hayo
na hatua zilizofikiriwa ilikuwa ni kuwa na Muungano utakaohakikisha
kuwapo kwa ulinzi wa kuinusuru Zanzibar isirejeshwe mikononi mwa Sultani
baada ya kupinduliwa.
Kupitia waasisi ambao ni Hayati Julius Nyerere na
Abeid Aman Karume kutoka kila upande wa Aprili 26,1964 wakaamua
kuchanganya udongo kama ishara ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
mnamo Aprili 26,1964 na kusaini Hati ya Makubaliano ya kuunda Tanzania.
Sababu nyingine za kulinda kisiwa hicho kupitia
Muungano ilikuwa ni kujenga umoja wa Wazanzibar baada ya kuonekana
mpasuko uliosababishwa na ubaguzi miongoni mwa Wapemba na Waunguja
ambapo hali inaonyesha bila Muungano, visiwa hivyo vingeweza kutengana
wakati wowote.
Pamoja na kuwapo Muungano, mpasuko baina ya
Uunguja na Upemba umeendelea kuonekana hadi leo na wakati wa kutoa maoni
ya Katiba Mpya, wapo waliosema wazi kuwa ziwepo Serikali nne,
wakimaanisha Serikali ya Unguja, Pemba, Tanganyika na ile itakayokuwa ya
Muungano.
Ieleweke kwamba hata busara ya makubaliano kati ya
Rais msaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF,
Maalim Seif Sharif Hamad kupitisha kura ya maoni kwa Wazanzibar na
kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inatokana na sababu ya kuimarisha
uhusiano kati ya Unguja na Pemba.
Pamoja na kubainika kwa upungufu mkubwa ukiwamo
kutonufaika na Muungano huo, inasemekana kuna makundi yanayotumiwa sasa
kisiasa na Sultani au wafuasi wake, kutaka kuuvunja Muungano wakati huu
wa kuandaa Katiba Mpya, ili kuirejesha Zanzibar mikononi mwao.
Hata hivyo, umuhimu wa Muungano huo unazidi kuwapo
na kuonekana kama ambavyo hayati Mwalimu alikuwa akisema mara kwa mara,
kuwa mgawanyiko huo ukiruhusiwa Zanzibar haitakuwa salama.
2 Comments